Skip to main content
Please wait...

Waziri wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Turathi azindua Kamati Andalizia ya Kusheherekea Siku ya Kiswahili Duniani afisini mwake. Maadhimisho hayo yatafanyika mnamo tarehe Saba mwezi wa Saba mwaka huu (7-7-2024).

Aidha, Kongamano la Kiswahili litafanyika kati ya tarehe tano hadi sita.

Yapo mambo kadha wa kadha yalijadiliwa kwenye kikao hiki yakiwemo: mahala ambapo sherehe hii itafanyika kukiwa na pendekezo la Mombasa, kadhalika kufanikisha sherehe hii kwa kukahikisha kuwa mataifa ya Afrika Mashariki yanakongamana.

Vilevile kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya lugha hii ya Kiswahili katika hafla hii. Kadhalika, kuratibu mambo ya itifaki na usalama.

Image
Image
Image
Image
Image
Image
Image
Image
Image